Ingia / Jisajili

Siku Ile Niliyokuita Uliniitikia

Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Richard Samson

Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 17 Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1. Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.

2. Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umekuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu. 

3. Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali. Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu.

4. Na mkono wako wa kuume utaniokoa. Bwana atanitimiliza mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa