Ingia / Jisajili

Jongeeni Bethlehemu

Mtunzi: Frt. Joseph Mwakapila
> Mfahamu Zaidi Frt. Joseph Mwakapila
> Tazama Nyimbo nyingine za Frt. Joseph Mwakapila

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Joseph Isaya Mwakapila

Umepakuliwa mara 1,464 | Umetazamwa mara 4,272

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio: Leo ni siku ya furaha Mwokozi wetu kazaliwa, waamini wote jongeeni mbele tumfanyie shangwe x 2.

Haya twende (twende), twende wote (twende), Bethlehemu (twende), tukamwone (twende), tumwabudu (twende), tumsujudu (twende), mtawala milele x 2.

  1. (a) Jeshi la malaika wanaimba kwa furaha, wanamsifu Mtoto aliyezaliwa.

(b) Mashariki Magharibi kaskazini kusini, wanamsifu Mtoto aliyezaliwa.

  1. (a) Tuungane na Maria Mama mtukufu wa Yesu; kumshukuru Mtoto aliyezaliwa.

(b) Na zawadi mikononi jongeeni Bethlehemu; kumshukuru Mtoto aliyezaliwa.

  1. (a) Kina baba kina mama kwa furaha nesa nesa; kwa ndelemo na vifijo msifuni Bwana.

(b) Watoto nanyi vijana ruka ruka kwa furaha; kwa ndelemo na vifijo msifuni Bwana.

  1. (a) Makasisi na watawa simameni tuwaone; pazeni sauti zenu msifuni Bwana.

(b) Watu wote duniani na muimbe na kucheza; pazeni sauti zenu msifuni Bwana.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa