Ingia / Jisajili

Usifiwe Moyo Mtakatifu Wa Yesu

Mtunzi: Frt. Joseph Mwakapila
> Mfahamu Zaidi Frt. Joseph Mwakapila
> Tazama Nyimbo nyingine za Frt. Joseph Mwakapila

Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu

Umepakiwa na: Joseph Isaya Mwakapila

Umepakuliwa mara 1,403 | Umetazamwa mara 3,891

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio: Usifiwe Moyo Mtakatifu wa Yesu, uliotuletea wokovu wetu x 2.

                Usifiwe (usifiwe) Utukuzwe (siku zote) nakuabudiwa na watu wote x 2.

  1. Moyo wa Yesu Moyo wa Mwana wake Baba wa milele,

             Moyo wa Yesu Moyo Hekalu takatifu lake Mungu.

  1.  Moyo wa Yesu Moyo liotungwa mwilini mwa Bikira,

              Moyo wa Yesu Moyo mwenye utukufu siopimika.

  1. Moyo wa Yesu Moyo hema yake Yeye Aliye juu,

             Moyo wa Yesu Moyo nyumba ya Mungu na mlango wa mbingu.

  1. Moyo wa Yesu Moyo unaojaa wema na mapendo,

             Moyo wa Yesu Moyo uliompendeza Baba kabisa.

  1. Moyo wa Yesu Moyo mwenye uvumilivu na huruma,

             Moyo wa Yesu Moyo mkarimu kwa wote waombao.

  1. Moyo wa Yesu Moyo malipo ya dhambi zetu wanadamu,

             Moyo wa Yesu Moyo furaha ya watakatifu wote.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa