Mtunzi: Felician Albert Nyundo
> Tazama Nyimbo nyingine za Felician Albert Nyundo
Makundi Nyimbo: Tenzi za Kiswahili
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 2,164 | Umetazamwa mara 6,514
Download Nota Download Midi1. Kilio changu ukikisikia, ufanye haraka kunisaidia,
Na pindi shida zinaponijia, ufanye haraka kunisaidia.
2. Ee Mungu wangu, ndiwe kimbilio, Ewe Bwana wangu, ndiwe tegemeo.
Nikitaabika uje kwangu mbio, Ewe ngome yangu, njoo kwangu, njoo.
3. Usinitupe wewe ndiwe kinga, Mimi ni kondoo, wewe wanichunga.
Adui zangu zidi kuwapinga, Na giza likija, nipatie mwanga.
4. Daima wewe ni wangu msaada, Bwana, usichoke zidi kunilinda.
Ukiwa nami sitapata shida, Kwa uwezo wako, mimi nitashinda,
5. Uniepushe na mwovu shetani, Ili asinitie majaribuni.
Mimi mnyonge nakutumaini, Wewe uwe nami, nifike mbinguni.