Ingia / Jisajili

Kimya Bara Na Bahari

Mtunzi: Fr. Gregory F. Kayeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Gregory F. Kayeta

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 17,884 | Umetazamwa mara 27,967

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kimya Bara na Bahari kimya mbingu na dunia / Bwana na muumba wetu mtoto Yesu asinzia.

2. Amelazwa manyasini  mchanga mkiwa pia mnyonge/ Yosefu na Mariamu wanamtunza mtoto Yesu.

3. Malaika wanashuka kumlinda mfalme wao / wanatunga nyimbo nzuri kumwimbia mtoto Yesu.

4. Wachungaji waja mbio  kwa mshangao waingia / waanguka magotini wamwabudu mtoto Yesu.

5. Nasi pia twende hima tukamwone Mungu wetu / twende sote kwa juhudi kumwamkia mtoto Yesu.


Maoni - Toa Maoni

Amani Mang'alila wa Dodoma. Dec 10, 2020
Wimbo Unaoishi, Hauishi Radha, Hauchoshi Kuuimba, Unatafakarisha na Umebebea Ujumbe Sahihi. Tangu Nikiwa Mtoto Nausikia na Sijawahi Uchoka. Asantee Sana Fr. Kayeta???

michael Oct 31, 2018
Winbo mzuri sana mungu akubariki

george joseph May 03, 2018
wimbo mzur sana mbarikiwe

AIDAN ADAM KAPINGA Dec 18, 2017
Mungu aendelee kubariki kazi ya mikono yako. Wimbo ni mzuri

Mkwalakwala May 28, 2017
Wimbo mzuri sana. Mungu abariki kazi ya mikono ya mtunzi

Toa Maoni yako hapa