Ingia / Jisajili

KUMBUKA REHEMA ZAKO EE BWANA

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 104 | Umetazamwa mara 159

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 26 Mwaka A

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Kumbuka rehema zako ee Bwana, kumbuka rehema zako ee Bwana(pia) kumbuka hata na fadhili zako. 1.Unijulishe njia zako, mapito yako unifundishe katika kweli uniongoze nifundishe ukweli maana ndiwe Mungu wa wokovu wangu. 2.Makosa ya ujana wangu, nayo maasi yangu yote ee Bwana usiyakumbuke unisamehe dhambi zangu zote, maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu. 3.Kadiri ya fadhili zako ee Bwana unatukumbuka, twajua njia nzako Bwana ndizo fadhili na ukweli maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu. 4.Bwana yu mwema na mwadili kwa hiyo anatufundisha sisi matakwa yake yote daima anatufadhili maana yeye ndiye Mungu wa wokovu wangu. 5. Wapole unawaongoza kwenye hukumu yako Bwana, wawafundisha njia zako ndizo fadhili na ukweli, maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa