Ingia / Jisajili

Kwa Furaha

Mtunzi: Nelson Wandabusi
> Mfahamu Zaidi Nelson Wandabusi
> Tazama Nyimbo nyingine za Nelson Wandabusi

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Nelson Wansabusi

Umepakuliwa mara 223 | Umetazamwa mara 774

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Kwa furaha tele nitaijongea meza yake Bwana (nile) chakula cha roho Kwa utii tele nitaishiriki karamu ya Bwana (ninye) kinywaji cha roho Mwili na damu (yake) ni chakula chetu (sisi) Alituachia (sisi) kiwe (ni)ukumbusho (wake kwetu) Tukikishiriki (sote) tutapata shibe (milele) Leo na milele (sote) tutapata shibe (milele) 2. Jenga urafiki, naye bwana Yesu, uje karamuye (ule) chakula cha roho Jilegeze ndugu, umkubali Yesu, uje karamuye (unywe) kinywaji cha roho 3. Ewe Bwana wangu, sistahili mimi, sema neno moja (roho) yangu itapona Japo ni dhaifu, na wingi wa dhambi, sema neno moja (roho) yangu itapona 4. Njoo kwangu Bwana, ninakuhitaji, nipate neema (tele) maishani mwangu Vita vya kiroho, wanipigania, ninakuhitaji (tangu) leo na milele

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa