Mtunzi: Ansert Mchefya
> Tazama Nyimbo nyingine za Ansert Mchefya
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Vusile Silonda
Umepakuliwa mara 1,246 | Umetazamwa mara 3,649
Download Nota Download MidiMacho yetu humwelekea Bwana Mungu wetu hata atakapo turehemu x 2.
Mashairi:
1. Nimekuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni, kama vile macho ya watumishi kwa mkono wa Bwana zao.
2. Kama macho ya mjakazi kwa mkono wa bibi yake, hivyo macho yetu umwelekea Bwana Mungu wetu hata atakapo turehemu.
3. Uturehemu Ee Bwana uturehemu sisi kwa maana tumeshiba dharau, nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, na dharau ya wenye kiburi.