Ingia / Jisajili

Magnificat

Mtunzi: Br. Charles Nachinguru, Ofmcap.
> Mfahamu Zaidi Br. Charles Nachinguru, Ofmcap.
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Charles Nachinguru, Ofmcap.

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Emmanuel Mwita

Umepakuliwa mara 1,095 | Umetazamwa mara 3,189

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

                MAGNIFICAT

Moyo moyo wangu wamtukuza Bwana x2

Na roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu x2

1. Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma/

    Mtumishi wake mdogo,*
    Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
    Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu,*
    Jina lake ni takatifu.
 
2. Huruma yake kwa watu wanaomcha*
    Hudumu kizazi hata kizazi.
    Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:*
    Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
 
3.  Amewashusha wenye vyeo kutoka viti vyao vya enzi,*
    Akawakweza wanyenyekevu.
    Wenye njaa amewashibisha mema,*
    Matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
 
4.  Amempokea Israeli mtumishi wake,*
     Akikumbuka huruma yake,
     Kama alivyowaahidia wazee wetu,*
     Abrahamu na uzao wake hata milele.
 
5.  Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,*
     Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele. Amina.
 
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa