Mtunzi: Fr. Amadeus Kauki
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Amadeus Kauki
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Fr. Amedeus Kauki
Umepakuliwa mara 2,648 | Umetazamwa mara 7,975
Download Nota Download MidiKiit: Moyo Wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inamshangilia Bwana Mwokozi wangu.
Viimbilizi:
Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma/
Mtumishi wake mdogo*
Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
Kwa kuwa mwenyezi Mungu amenitendea makuu,*
Jina lake ni takatifu.
Huruma yake kwa watu wanaomcha*
Hudumu kizazi hata kizazi.
Amefanya mambo makuu kwa mkono wake*
Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao.
Amewashusha wenye vyeo kutoka viti vyao vya enzi*
Akawakweza wanyenyekevu.
Wenye njaa amewashibisha mema*
Matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
Amempokea Israeli mtumishi wake*
Akikumbuka huruma yake.
Kama alivyowaahidia wazee wetu*
Abrahamu na uzao wake hata milele.