Ingia / Jisajili

Maria Mtakatifu

Mtunzi: Marcus Mtinga
> Mfahamu Zaidi Marcus Mtinga
> Tazama Nyimbo nyingine za Marcus Mtinga

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 12,902 | Umetazamwa mara 26,350

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

  1. Salamu Mama yetu Maria, Bikira na mwombezi wetu mwema
    Wewe ni kinga yetu, ni msimamizi wetu na Mama wa huruma ( Mama Maria )

    Maria mtakatifu, Mama wa Mkombozi tunalia sikia, tunalalamika; Maombi yetu Mama, uyasikilize na uyafikishe kwa mwanao Yesu x 2
     
  2. Njia hatuioni twendako hatujui maria taa yetu,
    Tulinde hatarini utufikishe vema Wewe ni ngao yetu ( Mama Maria..... )
     
  3. Safari yetu ndefu uchovu unazidi Mama tutie nguvu.
    Mawimbi ni makali dhoruba mvua kali Tunaishiwa nguvu ( Mama Maria..... )

  4. Nyosha mkono wako tukinge na mauti na dhambi tuepushe.
    Mlango tufungulie tumwone Yesu kristu Ee Mama tufikishe ( Mama Maria..... )


Maoni - Toa Maoni

Hedwiga Gussa May 04, 2018
hongera sana kwa kazi unayoifanya

jelance Sep 07, 2017
Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu

Amos Jun 02, 2017
bwana akuzidishie kipaji chako kiendelee!

joachim kulwa Jan 01, 2017
Mungu mwenyezi azidi kukubariki uzidi kuutangaza ufalme wake

Aloyce massawe Nov 09, 2016
Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu safi sana nampongeza mtunzi

Joachim John Nov 03, 2016
Nampongeze sana ndg Marcus Mtinga kwa kujawa na Roho wa Bwana,hata akampa maono ya utunzi wa huu wimbo.Tumuombe sana mwenyezi Mungu adizi kuwajalia neema wote wanaomkimbilia kwa moyo wa majitoleo.Amina

Phanice Bosibori Oct 24, 2016
nawapongeza sana na Mungu awape nguvu muendelee na utunzi. naomba nipate kanda zaidi

Toa Maoni yako hapa