Ingia / Jisajili

Najisifia Udhaifu Wangu

Mtunzi: Marcus Mtinga
> Mfahamu Zaidi Marcus Mtinga
> Tazama Nyimbo nyingine za Marcus Mtinga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 1,607 | Umetazamwa mara 4,121

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nitajisifia udhaifu wangu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristu ukae juu yangu maana ninapokuwa dhaifu ndipo nilipo na nguvu x2

  1. Sina budi kujisifia japo kuwa haipendezi, lakini ninajizuia nisihesabiwe hatia, bali nasema ukweli juu ya maono niliyopata.
  2. Sababu ya mafunuo hayo nalipewa mwiba mwilini, nikamsihi Mungu wangu jambo hili liniepuke, naye akaniambia neema yangu pekee inatosha.
  3. Napendezwa na udhaifu dharau taabu mateso, nakuyavumilia yote hayo kwa ajili ya Kristu, kwani uweza wa Kristu hutimia katika udhaifu.


Maoni - Toa Maoni

magambo Feb 24, 2018
nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya kwani mnasaidia watu wengi kupata nyimbo kiliturujia mimi binafsi nasema Asanteni na mzidi kufanya kazi ya mungu kwa uinjilishaji huo Asante!

Toa Maoni yako hapa