Ingia / Jisajili

Mbele Ya Miungu

Mtunzi: Roy Kimathi
> Tazama Nyimbo nyingine za Roy Kimathi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Roy Kimathi

Umepakuliwa mara 476 | Umetazamwa mara 2,050

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 5 Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mbele ya miungu

K) Mbele ya miungu nitakuimbia Zaburi

  1. Nitakushukuru kwa moyo wote kwa Moyo wangu wote, mbele ya miungu kweli nitakuimbia zaburi

Nitalisujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, hekaluni mwako nitalishukuru jina lako

  1. Nitalishukuru jina lako bwana kwa kuwa umeikuza, ahadi yako kuliko kulikuza jina lako

Uliniitika nilipokuita ulifariji nafsi yangu, kanitia nguvu Bwana ulinifariji moyo.

  1. ‘Falme wa dunia watakushukuru wakisikia maneno, ya kinywa chako maneno maneno ya kinywa chako

Wataimba njia zake Bwana Mungu kwa kuwa Bwana amejaa,utukufu mkuu naam wataimba njia zako


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa