Ingia / Jisajili

Mfalme Wa Amani

Mtunzi: Hajulikani
> Tazama Nyimbo nyingine za Hajulikani

Makundi Nyimbo: Matawi

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 6,013 | Umetazamwa mara 12,683

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  1. Mfalme wa amani mpeni heshima, Yerusalemu mjini anaingia,
    Na unyenyekevu na upole mkuu, anapanda punda Mwana wa Mungu

    Hosana Juu, Hosana Juu, Hosana Juu x 2

  2. Njoni Mahebruni njoni watoto, leteni matawi ya kumsalimu,
    Mwana wa Daudi kweli masiha, anakuja kwetu mwenye huruma.

  3. Tandikeni nguo miguuni mwake, imbeni zaburi shangilieni,
    Mbarikiwa huyu ajaye kwetu, kwa jina la Bwana mkombozi mkuu

  4. Ufurahi sana we Yerusalemu, yule mwabudu roho za mbingu,
    Na huruma pole anakujia, alete amani kukutuliza

  5. Ndimi za wachanga zafumbuliwa, kwa miujiza yake masiha,
    Na makundi yote ya malaika, sifa na heshima wanamtolea.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa