Mtunzi: Mmole G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Mmole G.
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Gereon Mmole
Umepakuliwa mara 688 | Umetazamwa mara 2,409
Download Nota Download MidiKiitikio
Mimi ndimi mkate wa uzima asema Bwa na, mimi ndimi mkate wa uzima yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. x2
Viimbilizi
1. Yesu anasema, Baba yangu anawapa ninyi, chakula cha kweli kitokacho mbinguni.
2. Amini Amini, msipoula mwili wake Mwana wa Adamu, na kuinywa damu yake hamna uzima ndani yenu.
3. Aulaye mwili wangu, nakuinywa damu yangu, anao uzima wa milele nami nitamfufua siku ya mwisho.
4. Aulaye mwili wangu, nakuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu nami hukaa ndani yake.