Mtunzi: Benny Weisiko John
> Mfahamu Zaidi Benny Weisiko John
> Tazama Nyimbo nyingine za Benny Weisiko John
Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu
Umepakiwa na: Benny Weisiko
Umepakuliwa mara 869 | Umetazamwa mara 3,403
Download Nota Download MidiKIITIKIO
Moyo Mtakatifu wa Yesu Kristo (Ewe) uliye msimamizi (na somo) wa kwaya yetu, utuhurumie sisi wanao.
Moyo Mtakatifu wa Yesu Kristo (Ewe) uliye msimamizi (na somo) wa kwaya yetu, utupiganie sisi wanao.
[Tunapokusanyika (kwa pamoja) mahali popote (Yesu),
Tunapokusanyika (kwa pamoja) uwe kati yetu (daima) utukinge kwa Damu yako dhidi ya shetani mwovu.]x2
SHAIRI (ALTO &SUPRANO)
1.Kwa Damu yako Takatifu Ee Yesu, utupe nguvu tushinde vishawishi, tukutumikie wewe kwa sauti za kuimba, (daima) tutangaze neno lako kwa kuimba.
2. Utujalie tudumishe upendo, tuwasamehe wanaotukosea, utujalie baraka katika maisha yetu, (nasi) tutembee kwa furaha ndani yako
SHAIRI (TENO & BASS)
3. Sauti zetu hizi zinazovuma kwa kishindo, ziambatane na nguvu zako kutoka Mbiguni,
ziwashe moto hapa katikati yetu, zifukuze giza pia na pepo wachafu, Njoo Yesu kaa nasi.