Mtunzi: Joseph C. Shomaly
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph C. Shomaly
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 3,495 | Umetazamwa mara 6,049
Download Nota Download Midi1. Tunayapiga makofi na nyimbo za sifa,
Tunashangilia, tunafurahia
Leo tunasisimka kumshukuru Muumba
<h4>
Huo - ndio kweli, msisimko wa si-fa kweli
Pepo - na shetani wameshatimua mbi-o kweli
Tuna-lipa sifa jina lake Yesu Kri-stu kweli
Nasi - twamsifu Mungu kwa shangwe na si-fa
{ Sisimka (sisimka) sisimka (sasa sisimka)
Shangilia (tuimbe wote) Jina Yesu
Tumeuona wema wake na mkono wake umetubariki } *2
</h4>
2. Jua linapochomoza jogoo kawika,
Mungu katupenda, anatuamsha
Leo tunasisimka kumshukuru Muumba
3. Mvua nayo inanyesha sisi hatujui,
Imetoka wapi, mapenzi ya Mungu
Leo tunasisimka kumshukuru Muumba
4. Vyakula tunavyokula vinatupa nguvu,
Twatembea vyema, na akili nyingi
Leo tunasisimka kumshukuru Muumba
5. Majira nazo nyakati azipanga Mungu,
Sisi tunaishi, kwa mapenzi yake
Leo tunasisimka kumshukuru Muumba