Mtunzi: Joseph C. Shomaly
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph C. Shomaly
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 8,224 | Umetazamwa mara 13,274
Download Nota Download MidiMISA UPENDO – J. C. SHOMALY
BWANA UTUHURUMIE
{Bwana, Bwana, utuhurumie
Ee ee Bwana utuhurumie,
Ee Bwana (ee Bwana) , ee Bwana (ee Bwana)
Ee Bwana (ee) Bwana utuhurumie Bwana } *2
/s/ {Kristu- Kristu utuhurumie,
Kri-stu utuhurumie } *2
/a/ Kristu Kristu utuhurumie,
Ee Kri-stu utuhurumie
/t/ Ee Kristu, ee Kristu Kristu
Ee Kristu kri-stu utuhurumie
/b/ Ewe Kristu Kristu- Kristu Kristu
Kri-stu (Kristu) utuhurumie
3. Bwana Bwana utuhurumie . . .
UTUKUFU (MISA UPENDO)
{Utukufu kwa Mungu juu (utukufu )
Na amani duniani
Kwa watu wote (watu wote)
Wenye mapenzi (penzi mema)
(iyo) kwa watu wote, wenye mapenzi
Mapenzi mema (utukufu) } *2
1. Tunakusifu, tunakuheshimu,
Twakuabudu, tunakutukuza
Tunakushukuru, Mungu kwa ajili,
Ya utukufu, wako mkuu
Ee Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni
Mu-ngu Baba, Mungu Mwe-nyezi
Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee,
Ee Bwana Mungu, ee Bwana Mungu
2. Mwanakondoo, mwana wake Baba,
Uondoaye, dhambi za dunia
Utuhurumie, utuhurumie,
Pokea ombi, letu ee Baba
Mwenye kuketi, kuume kwa Baba,
Tuhurumie, utuhurumie
Kwa kuwa kwa kuwa, ndiwe peke yako,
Mtakatifu, Mtakatifu
3. Pekee Bwana, mkuu Yesu Kristu,
Pamoja naye, Roho Mtakatifu
Katika katika, utukufu wake,
Mu-ngu Baba, a-mina.
MTAKATIFU
Mtakatifu mtakatifu Bwana (Mungu)
Mungu wa majeshi, Mungu wa majeshi
Mbingu na dunia zimejaa, utukufu wako
[sop]
Hosanna, Hosanna,
Hosanna juu, ho-sanna juu Mbinguni
[alto]
Hosanna hosanna hosanna *2
Hosanna hosanna oo
Hosanna juu mbinguni
[tenor]
Hosanna, hosanna,
Hosanna ho—sanna juu mbinguni
[bass]
Hosa-nna, hosa—nna
Hosanna ho—sanna juu mbinguni
Mbarikiwa anayekuja
Kwa jina la Bwana
107. MWANAKONDOO
{Mwanakondoo wa Mungu,
Uondoaye dhambi za dunia
Ee Mwana, tuhurumie } *2
Mwa-nakondoo mwana wa Mungu
Uondoaye dhambi dhambi za dunia,
{Tupe amani (amani) tupe amani
Tupe amani } *2