Ingia / Jisajili

Msisumbukie Maisha Yenu

Mtunzi: Lucas Mlingi
> Mfahamu Zaidi Lucas Mlingi
> Tazama Nyimbo nyingine za Lucas Mlingi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: lucas mlingi

Umepakuliwa mara 631 | Umetazamwa mara 2,948

Download Nota
Maneno ya wimbo

KIITIKIO; Msisumbukie maisha yenu mtakula nini? mtavaa nini? //kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula na mwili nao mwili ni zaidi ya mavazi x2

SHAIRI. 1 Waangalieni ndege wa angani hawapandi wala hawavuni, hawakusanyi ghalani, Baba yenu wa Mbinguni huwalisha hao Je! ninyi si bora kuliko hao. kiit.......

2. Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua yeye aweza kujiongezea kimo chake, japo kiasi cha mkono mmoja.

3. Na mavazi ya nini kuyasumbukia fikirini maua ya mashambani (hayafanyi kazi wala hayasokoti nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa