Mtunzi: B.p.mwandu
> Mfahamu Zaidi B.p.mwandu
> Tazama Nyimbo nyingine za B.p.mwandu
Makundi Nyimbo: Watakatifu
Umepakiwa na: Beatus Mwandu
Umepakuliwa mara 692 | Umetazamwa mara 2,705
Download Nota Download MidiSalamu ewe somo wa kwaya yetu Mtakatifu Karol Lwanga. Mwombezi na msimamizi wetu mwema toumbee kwa Mungu Baba. Katika utume wa uimbaji, tuweze kutangaza injili kwa imani na matendo. Tuige mfano wako mwenyewe, na mwisho tufike mbinguni kwa Baba we uliko.
1.Tujaliwe moyo wa mapendo,tumpende Mungu, na tupendane sisi kwa sisi.
2.Tuitetee imani yetu, tuziishi vema sakramenti, tukimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
3.Tutimize wajibu wetu kwa kanisa. Tuwe kielelezo bora kwa jamii. Maisha yetu yamshuhudie Kristo,huo ndio uinjilishaji wa kweli.