Mtunzi: Furaha Mbughi
> Mfahamu Zaidi Furaha Mbughi
> Tazama Nyimbo nyingine za Furaha Mbughi
Makundi Nyimbo: Anthem | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Furaha Mbughi
Umepakuliwa mara 22 | Umetazamwa mara 41
Download Nota Download MidiMTINI By
F.Mbughi
Yesu alipokuwa kule
Bethania, aliona njaa; kwa mbali akauona Mtini wenye majani, akaenda ili labda
aone kitu juu yake. Na alipo ufikia hakuona kitu ila majani, maana si wakati wa
tini.
Yesu akaujibu akauambia,
{“Tangu leo hata milele, mtu asile matunda kwako”}x2.
Na asubuhi walipokuwa
wakipita, {waliuona ule mtini, ule mtini umenyauka, umenyauka toka shinani}x2
Petro akakumbuka habari
yake akamwambia, {Rabi, Rabi, tazama ule mtini ulio ulaani umenyauka}x2
Yesu akajibu akamwambia,
mwamini Mungu, mwamini Mungu, amin nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu
ng’oka, ngo’ka, ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini
kwamba hayo ayasemayo yametukia, nayo yatakuwa yake.
{Kwasababu hiyo, nawaambia,
nawambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa
yenu}x2.