Ingia / Jisajili

Mungu Mkuu

Mtunzi: Daniel P. Mnyawi
> Mfahamu Zaidi Daniel P. Mnyawi
> Tazama Nyimbo nyingine za Daniel P. Mnyawi

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Daniel Mnyawi

Umepakuliwa mara 121 | Umetazamwa mara 378

Download Nota
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Ee bwana Mungu mkuu sana mwenye kutisha, ashikaye maagano kwao wampendao. Tumetenda dhambi bwana tumefanya uovu, tumekukaidi tumekuasi kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako. Mashairi: 1. Hatukusikiliza watumishi wako manabii ambao walisema nasi, na mababu zetu kwa jina lako. 2. Rehema msamaha ni kwa Mungu wetu, ingawa tumemwasi ni mwingi wa rehema. Tuepushe bwana na ghadhabu yako. 3. Ee Mungu usikie tega sikio lako, fumbua macho yako tazama ukiwa wetu. Ee bwana tusamehe kwa uovu wetu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa