Ingia / Jisajili

Mwana wa Seremala

Mtunzi: Sylvanus Mpuya
> Mfahamu Zaidi Sylvanus Mpuya
> Tazama Nyimbo nyingine za Sylvanus Mpuya

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 369 | Umetazamwa mara 1,425

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1.Na alipofika Bwana Yesu katika nchi yake, akafundisha na kufanya Miujiza kwenye sinagogi hatawakashangaa wakasema.

Kiitikio:

Huyu amepata wapi Hekima hii na miujiza hii x2. {Huyu si mwana wa Seremala huyu si mwana wa Seremala huyu si mwana wa Seremala! x2}

2.Mamaye si yeye, si yeye aitwaye Mariamu, na ndugu zake si Yakobo Yusufu na Simoni na Yuda hata wakashangaa wakashangaa wakasema.

3.Na maumbu zake, hawa wote hawapo hapa petu, basi huyu basi huyu amepata wapi haya yote hata wakashangaa wakashangaa wakasema.

4.Wakuchukizwa naye Yesu akawaambia nabii hakosi heshima ila katika nchi yake na nyumbani mwake yeye nyumbani wake mwenyewe.

5.(Bwana Yesu) wala hakufanya, Miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kutokuamini kwao hakika,(Bwana Yesu) wala hakufanya, Miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kutokuamini kwao naye Yesu, (Bwana Yesu) wala hakufanya, Miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kutokuamini kwao 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa