Ingia / Jisajili

Naja Kwako Baba

Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi

Makundi Nyimbo: Mazishi

Umepakiwa na: FRED KITUYI

Umepakuliwa mara 1,123 | Umetazamwa mara 5,711

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NAJA KWAKO BABA (F.B. KITUYI)

Kiitikio:

Mungu Baba naja kwako Baba unipokee, kweli mimi mkosefu, usinikatae. x2

Nakuomba Baba mwema u mwingi wa huruma, kweli mimi mkosefu, usinikatae. x2

  1. Nimezongwa nazo dhambi, sina wema mbele zako;

(Mimi mdhaifu Baba, unihurumie kweli x2)

  1.  Nikisema sina dhambi, nadanganya mbele zako;

           (Nimekosa mbele zako, ninaona haya kweli. x2)

  1.    Nimewacha njia zako, nikaenda kombo kombo;

             (Sikufai kitu kamwe, unihurumie kweli. x2)

  1.  Kama ungezihesabu, dhambi zetu Mungu Baba;

            (Nani angekuja kwako, asimame mbele zako. x2)

      5.   Wewe mwingi wa rehema, si mwepesi wa hasira;

          (Nimetenda dhambi Baba, nipokee naja kwako. x2)


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa