Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 885 | Umetazamwa mara 2,761
Download Nota Download MidiWEWE NI MTEULE – F.B.B KITUYI
Kiitikio
Wewe ni mteule wangu, wewe ni mteule wangu, mjumbe wangu,
njoo nikutume mpendwa wangu njoo. x2
Shambani mwako Bwana mna kazi nyingi (mbali mbali),
Kazi ni nyingi, lakini watenda kazi kweli ni wachache,
Lakini watenda kazi kweli ni wachache. x2
1. Bwana tuma watenda, Ee Bwana tuma watenda kazi,
Kwani mavuno mengi lakini, watenda kazi wachache.
2. Bwana akikuita, itika kweli usikatae,
wewe ni mtumishi wa Bwana,
enenda shambani mwake.
3. Hubiri kwa kuimba, hubiri na kwa maneno pia,
na kwa vitendo vyako hubiri, hubiri usiogope.
4. Bwana yuko na wewe, shetani hatakushinda
kamwe, mkono wa kuume wa Mungu,
umekuzunguka wewe.