Mtunzi: Deo Kalolela
> Mfahamu Zaidi Deo Kalolela
> Tazama Nyimbo nyingine za Deo Kalolela
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 5,418 | Umetazamwa mara 12,699
Download Nota Download Midi
D. KALOLELA.
Naja kwako Bwana wangu naomba shime yako nifungulie milango Bwana ya nyumba yako leo.
(Natamani sana Bwana mimi niwe mtumishi wako, niongoze Bwana wangu ili nifike kwenye meza yako) x 2
1. Nishike mkono Bwana niongoze kwenye Altare yako, niongoze Bwana wangu nisipotee. Ninatamani sana kufika kwenye altare yako Bwana lakini kwa nguvu zangu siwezi kitu.
2. Tazama kondoo zako duniani walivyotawanyika, moyo wangu uko radhi kuongoza kondoo zako Bwana, nIchague mimi Bwana niwakusanye, na kwa fimbo yako Bwana nisaidie.
3. Kwa nguvu zako Ee Bwana nijalie Imani kamilifu, nipe moyo wa huruma na mapendo na wa uvumilivu, nivishinde na vikwazo vya shetani, niwe mkarimu Bwana kwa kundi lako