Ingia / Jisajili

NAJONGEA

Mtunzi: Teddy Wambua
> Mfahamu Zaidi Teddy Wambua
> Tazama Nyimbo nyingine za Teddy Wambua

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Teddy Wambua

Umepakuliwa mara 400 | Umetazamwa mara 1,391

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NAJONGEA

KIITIKIO

Naja mbele zako Bwana najongea kwenye altare (yako) (Bwana wangu) nikupokee wewe Bwana kwa mwili na damu

Njoo kaa ndani yangu Bwana mimi nifarijike (ili) (Bwana wangu) niishi nawe Yesu uniongoze daima

Sop-(Karibu Yesu mwokozi wangu,ukae ndani yangu,ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2

Alto-(Karibu Yesu,ukae ndani,ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2

Tenor-(Karibu Yesu mwokozi wangu,ukae ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2

Bass-(Karibu Yesu wangu ukae ndani yangu,uiguze roho yangu na ikutii)×2

MASHAIRI

1.Bwana nishibishe na chakula hicho cha roho,unishinishe siku za maisha yangu yote

2.Nafsi yangu yakuonea kiu wewe Bwana,uninyweshe nisione kiu milele yote

3.Katu sikustahili kuijongea altare,unihurumie nipokee mwengi wa rehema

4.Niishi kiekaristia hadi nikate roho,mwisho nifufuke niishi nawe milele yote



Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa