Mtunzi: Teddy Wambua
> Mfahamu Zaidi Teddy Wambua
> Tazama Nyimbo nyingine za Teddy Wambua
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Misa | Shukrani
Umepakiwa na: Teddy Wambua
Umepakuliwa mara 348 | Umetazamwa mara 1,518
Download Nota Download MidiTABASAMU LA UPENDO
Mashairi
Sop/Alto
1.Ingawa ni mwepesi wa kusahau Bwana nifundishe upendo,maana wewe Mungu muumba wa vyote wewe mwenyewe upendo,
Ukaniumba mimi kwa mfano wako kudhihirisha upendo, ukamtoa mwana wako wa pekee Yesu afe kwa ajili yangu,
2.Nijinyime anasa kukutumikia wewe huo ni upendo,neema rehema furaha faraja vyote nijaze kwa upendo,
Kila nikikutafakari nikiwaza nikumbuke upendo,mawazo yangu (ya) daima yawe yamezingirwa na upendo,
KIITIKIO
Sop:(Bwana unipe upendo unijaze upendo,nami nihubiri upendo kwa walimwengu nasi Bwana,utubariki na tuweze kupendana daima tutabasamu tabasamu la upendo (wa)×2 wako.
Alto:(we Bwana unijaze upendo,nihubiri kwao walimwengu nasi,we Bwana tubariki na tupendane,daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wako.
Tenor:(Bwana Mungu wangu nijaze upendo kama ulivyo nami nihubiri upendo kwa walimwengu upendo Bwana tubariki na tabasamu lako daima tutabasamu tabasamu la upendo (wa)×2 wako.
Bass:(Bwana unipe upendo unijaze upendo nihubiri upendo kwa walimwengu nasi Bwana tubariki tuweze kupendana na tutabasamu tabasamu la upendo wako)×2.
KIBWAGIZO
Tenor:1.popote ninapoenda mataifa yakiri upendo wake
:2.njia zote nipitazo zilindwe zikingwe nazo nguvu zake
Sop:Bwana aliyejaa neema na upendo ae
Alto:aliyejaa upendo ae
Tenor:Bwana aliyejaa neema na upendo ae
Bass:Bwana aliyejaa neema na upendo ae
Alto:1.naam upendo wake Bwana nivumishe kwayo
:2.naam na nguvu za shetani mwovu na zishindwe
Sop:(nasi tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wa
Alto:(daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2
Tenor:(daima tutabasamu tabasamu la upendo)×2
Bass:(tutabasamu tabasamu la upendo)×2 wako
*Baada ya kibwagizo rudi kwenye kiitikio*