Ingia / Jisajili

Nitamuimbia Mungu

Mtunzi: Teddy Wambua
> Mfahamu Zaidi Teddy Wambua
> Tazama Nyimbo nyingine za Teddy Wambua

Makundi Nyimbo: Misa | Shukrani

Umepakiwa na: Teddy Wambua

Umepakuliwa mara 466 | Umetazamwa mara 1,759

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

UTANGULIZI

Kama vile Daudi alivyomtukuza Mungu,akayavua mavazi yake ile amchezee

Ndivyo nami nitakavyomtukuza Mungu wangu,kwa sauti tamu nyororo yangu nikimsifu

KIITIKIO

Sop/Alto-Nitamuimbia Mungu wangu milele,nitampa sifa shangwe milele,(siku,wiki,miezi miaka,nafsi yangu itamsifu milele yote)×2

Tenor-Nitamuimbia Mungu,milele yote nitampa sifa shangwe milele,(siku Bwana,wiki miezi miaka yote,nafsi yangu msifu milele yote)×2

Bass-Nitamuimbia Mungu wangu milele,nitampa sifa shangwe milele,(siku na wiki miezi miaka yote,nafsi yangu msifu milele yote)×2

MASHAIRI

1.Alinijua hata kabla nizaliwe(mimi),(na) ananiongoza kwa yote hadi leo,milele apewe sifa na utukufu

2.Ananilinda usiku pia mchana(mimi),(na) ananijalia hayo ninayohitaji,milele apewe sifa na utukufu

3.Kipaji cha uimbaji yeye kanipa(mimi),(na) nitakitumia vizuri kumsifu,milele apewe sifa na utukufu

Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa