Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,435 | Umetazamwa mara 5,134
Download Nota Download MidiKiitikio:
Bwana sasa ninakuja (kwako) naomba unipokee (e bwana), japo mimi ni mdhambi (tena) kiumbe dhaifu sana (kwani) najua kwamba sistahili mbele zako lakini ninakusihi sana (e bwana) bwana nipokee (x2)
Mashairi:
1. Kwenye makao yako bwana unikaribishe, penye neema zako usisite kuniita, unipe tumaini lako (bwana) niwapo kwenye shida, uwe nami siku zote ninapokuhitaji
2. Nitakukabidhi maishi yangu bwana uyabadilishe, nitakukabidhi moyo wangu uufanye uwe mpya, nitajikabidhi kwako siku zote za maisha yangu, bwana nakusihi sana unipokee.