Ingia / Jisajili

Natamani Kujongea

Mtunzi: A. J. Msangule
> Tazama Nyimbo nyingine za A. J. Msangule

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Gervas Kombo

Umepakuliwa mara 3,439 | Umetazamwa mara 7,005

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Natamani kujongea kwenye altare ya Mungu wangu ili nami nishiriki kwenye karamu ya Bwana Yesu x2

Ni uone uzuri wa Bwana uliomo katika fumbo takatifu la Ekaristi mwili na damu ya Yesu Nimpokee Bwana Yesu Kristu na kuishi pamoja nae siku zote akae ndani yangu nami ndani yake

1.       Bwana naomba unijalie moyo wa uchaji nitubu dhambi nami nijongee meza yako

Ninakuomba unijalie usafi wa moyo nikupokee nikiwa katika hali njema

2.       Karamu yako ni takatifu tena ya amani iliyojaa upendo na uzima milele

Na wale watakao shiriki kwenye meza imewapasa kujua vema siri yako

3.       Uwajalie huruma yako na mapendo yako uwatie nguvu wote wasio kupokea

Kwa nguvu yako uwainue walioanguka waondoe vizuizi vinavyo waangusha

4.       Uwaalike wanao wote kwenye meza yako waishiriki karamu ya uzima wa milele

Wafurahie amani yako na mapendo yako yaliyofichwa kwenye fumbo hili takatifu


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa