Ingia / Jisajili

Ninakuabudu Mungu Wangu

Mtunzi: Joseph Makoye
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Makoye

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 10,657 | Umetazamwa mara 21,821

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1. Ninakuabudu Mungu wangu, Unayejificha altareni
Ninakutolea moyo wangu, usiofahamu siri yako.

2. Mafahamu yangu yadanganya, Yanapokuona na kugusa
Namsadiki Yesu hadanganyi, Yeye Mungu Mwana na ukweli

3. Waficha Umungu msalabani, Na ubinadamu altareni
Nami na ungama yote mbili, Kama mwivi yule mwenye toba.

4. Thomaso aligusa majeraha, Nami nasadiki bila shaka
Ewe Yesu nipe pendo lako, Tumani kwako na imani

5. Umeteswa nini Bwana mwema, Kwa kunipa mkate wa uzima
Yesu unifiche ndani yako, Ili nilionje pendo lako

6. Yesu Pellicane utazame, Na kwa damu yako nitakase
Tone moja ndilo linatosha, na dunia yote yaokoka

7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo, Utafunguliwa kwangu lini?
Nikuone Yesu uso wako, Nishiriki nawe heri yako

Amina, Amina


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa