Mtunzi: Paschal Florian Mwarabu
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Florian Mwarabu
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Gervas Kombo
Umepakuliwa mara 10,356 | Umetazamwa mara 20,621
Download Nota Download MidiPF MWARABU
1. Na hangaika hapa duniani maisha yangu hayana furaha najua wazi hapa si nyumbani bali njia ya kupita
Niongoze vema Maria mwema bondeni huku niliko nifike kwa usalama mbinguni kwa Yesu mwanao x2
2. Vita na shari vyote vyanisonga mashaka mengi yamenijia mwili na roho havina kinga hatari imezidi
3. Mama Maria ndiye jibu langu hapa safarini unisaidie uniombee kwa mwanao Yesu anikinge anilinde
4. Kwa kuwa Yesu ni mwokozi wangu nakusihi Mama nakusihi sana nifikishe kwake shida zangu unionee huruma