Ingia / Jisajili

Nitakutukuza Ee Mungu

Mtunzi: Julius Mokaya
> Tazama Nyimbo nyingine za Julius Mokaya

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Julius Mokaya

Umepakuliwa mara 1,205 | Umetazamwa mara 3,085

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nitakutuza Ee Mungu

Nitakutukuza wewe Ee Mungu,(Mungu wangu), kwa kuwa umeniinua;(juu),

hukuacha adui zangu,(Ee Mungu) washangilie juu yangu.

  1. Ee Bwana wangu, nilikuita unisaidie; na wewe umeniponya.
  2. Bwana umenitoa kuzimuni, umeniokoa nisishuke; kwenye shimo la mauti.
  3. Mwimbieni Bwana enyi watakatifu wake, lisifuni jina lake takatifu; mkikumbuka utukufu wake.
  4. Ee Bwana uliponijalia, uliumarisha mlima wangu; ukijificha ninafadhaika.
  5. Wageuza maombolezo yangu, nayo yakawa kicheko cha kweli; wanivika nguo za furaha.
  6. Hivyo moyo wangu utakusifu, kukaa kimya mimi sitaki; Bwana nitakushukuru milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa