Mtunzi: Noelle Hulk
> Mfahamu Zaidi Noelle Hulk
Makundi Nyimbo: Majilio
Umepakiwa na: Noelle Hulk
Umepakuliwa mara 3 | Umetazamwa mara 6
Download NotaNjoo kwetu njoo kwetu masiha, njoo utuondoe dhambini ×2
njoo masiha, njoo utuokoe, njoo utuondoe dhambini ×2.
1 .
(a) sop/Alto
Giza limetanda dunia yote, watu nao wamemwacha Mungu.
(b) ten/bass
Hima Bwana njoo utuokoe, sisi wanao twakuomba.
2.
(a). Mwenyezi Mfalme tunakungoja, utuondolee maumivu,
(b). Turudishe kwako tubadilike, njoo masiha tuokoe.
3.
(a). Njoo utuondoe utumwani, dhambi na mauti ziondoe.
(b). Milele na milele tuje kwako, njoo masiha tuokoe.