Mtunzi: Traditional
> Tazama Nyimbo nyingine za Traditional
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 9,388 | Umetazamwa mara 14,550
Download Nota Download Midi1. Malaika kaleta noeli ya kwanza kwa wachunga kondoo katika makonde, Betlehemu wakawa walinzi wazamu wakaona usiku maajabu ya nuru, (Noeli, Noeli, Noeli Yesu yu Mungu na binadamu) x 2.
2. Wakaona Mbinguni mwangaza wa nyota, Ing'aayo kwa mbali na masharikini, wakaenda upesi walivyoambiwa, Betlehemu wamwone mwokozi horini, Noeli, noeli..........................................
3. Mashariki watoka Wafalme watatu, Mamajusi waliotafuta Mfalme, Wafuata hii nyota walioiona, wasipate kumkosa wanayemtafuta. Noeli, Noeli.......................
4. Kiongozi ni nyota iliyowaleta hata mji wa Daudi alimozaliwa, Ikakaa mara moja isiendelee, palepale nyumbani alimo mwokozi, Noeli, Noeli................................
5. Basi sisi Wakristu na tumsujudie, tumhimidi Mwokozi aliyeviumba vitu vyote Mbinguni duniani, na sisi ametufia na kutukomboa, Noeli, Noeli...................................................