Ingia / Jisajili

SABATO

Mtunzi: Frederick Ajali
> Mfahamu Zaidi Frederick Ajali
> Tazama Nyimbo nyingine za Frederick Ajali

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Fredrick Ajali

Umepakuliwa mara 224 | Umetazamwa mara 1,246

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Yesu alikuwa akipita katika shamba, shamba la ngano siku ya sabato, wanafunzi wake wakaona njaa wakaanza kukwanyua masuke ya ngano wakala punje zake. Mafarisayo walipoona hayo wakamwambia Yesu, tazama wanafunzi wanakiuka sheria ya sabato. Yesu kawajibu, je? Hamsoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake walipokuwa na njaa. CHORUS: (Mafarisayo×2) walishika sheria ya sabato, wakamsahau Mungu mwenye sabato! Mafarisayo.... 2. Siku nyingine ya sabato, Yesu aliingia sinagogi akafundisha, mle ndani mlikuwa na mtu ambaye mkono wake, mkono wa kuume ulikuwa umepooza. Walimu wa sheria wakitafuta kisingizio, wakawa wanangojea waone kama atamponya. CHORUS: (Mafarisayo!×2) walishika sheria ya sabato, wakamsahau Mungu mwenye sabato! Mafarisayoo.. HITIMISHO: Basi nawaambieni kwamba pana kikubwa kuliko hekalu, laiti mngalijua maana ya maneno haya. Nataka huruma wala si tambiko×2 Hayo ni maneno ya Yesu×3 Hayo!.....

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa