Ingia / Jisajili

SAFARI MOJA

Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Derick Wafula

Umepakuliwa mara 7,981 | Umetazamwa mara 13,111

Download Nota
Maneno ya wimbo
*SAFARI MOJA*
      _@Bernard Mukasa_

1. Twajua Mbingu iko mbali na njia ndefu,  tena mitego ni mingi kila kona, lakini tumaini liko karibu nasi, kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu,  Naye atatuongoza tukimwamini, mpaka tufike salama tuendakoo. 

Safari ni moja tena na njia ni moja (aa) 
Hatua ni moja  moja foleni ni moja(naa)
Mlango mmoja tena mlango mwembamba, (twendee) twende tuingie tukaishi huko milele x2

2.Shetani hakuanza leo kutuvuruga,  tangu pale kwenye mti bustanini, kavunja ujamaa mwema wa Babu zetu, wakamkosea Mungu Wakaanguka, nao wakajihukumu wakajificha, wakitaka wapotee mbali naye. 

3.Ya Mbingu yakajinyenyekeza duniani,  Laana  ikatakaswa kwa sadaka,  ya mti yakavunjwa vunjwa juu ya mti, ya bustanini yakashindwa mlimani,  aibu ya Mwanadamu ikaondoka, akaandaliwa Ufalme Mbinguni.  

T/B: Tutazame mbele na tusigeuke nyuma,  Mwokozi wetu Yesu Anatungojea. 

Wote: Safari ni moja safari  moja,
Twendeeni pamoja safari moja,
Ipande milimani ni moja safari moja, 
Ishuke Mabondeni ni moja safari moja, 
Inyeshe liwake ni moja safari ni moja tuu.

Maoni - Toa Maoni

Michael Otieno Apr 16, 2020
Kazi njema Bwana Mukasa ila naomba kujua jinsi naezapata Audio ya huu wimbo Safari Moja. Nimeutafuta mtandaoni bila mafanikio. Shukran

Tesha Paul Aug 23, 2019
Best composer Bernard Mukassa Gusaneni majeraha

Toa Maoni yako hapa