Ingia / Jisajili

Sasa Wakati Umefika

Mtunzi: Lukando Andrew Basil
> Tazama Nyimbo nyingine za Lukando Andrew Basil

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Philemon Kajomola

Umepakuliwa mara 36,318 | Umetazamwa mara 49,445

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Sasa wakati umefika wa kushika nilichonacho (mimi) 
Kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi 
Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu 
(Ili) Aone nilivyoandaa zawadi ya leo 
Nitamwambia Bwana pokea hiki kidogo nilichonacho 
Kwani Mungu wewe wanijua mimi siwezi hata kueleza 
Nakusihi sana Baba unipokee 
Nigawie na baraka niwe salama

 

  1. Mema yote niliyokuwa nayo yametoka kwa Mungu 
    Hivyo nami ni kosa kusahau kumshukuru 
    Kwani kuwepo hapa leo hii ni kazi ya nani 
    Kamwe mimi sitapata uwezo pasipo Mungu 
  2. Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi 
    Mbona hofu yazidi kuwa ndani ya moyo wangu 
    Mbele ya Bwana Mungu wangu kufanya siri ni bure 
    Yeye ndiye mpanga mambo yote ya wanadamu 
  3. Pumzi anayonipa uhai unatoka kwa nani 
    Bila Mungu hakika mwanadamu siwezi kitu 
    Nimepata nafasi hii leo ya kwenda kutoa zawadi 
    Heri niende ya kesho sio yangu ajua Mungu

Maoni - Toa Maoni

Moses ndiu musava Feb 05, 2023
Chathelc

Nivard S. Mwageni Jan 03, 2020
Hongera kwa mtunzi. Melody imeishi kwa miaka mingi sana. Na ndio nyimbo ambazo kanisa linahimiza zitumike maana kanisa zima wanashiriki.

Jennifer mponda Oct 23, 2019
Wimbo ni mzuri mno. Unatukumbush

Toa Maoni yako hapa