Ingia / Jisajili

SHAMBA LA MIZABIBU LA BWANA

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 688 | Umetazamwa mara 2,135

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Shamba la mizabibu la Bwana, ndilo nyumba ya Israeli ndilo nyumba ya Israeli shamba la Bwana ndilo nyumba ya Israeli. 1a).Wewe uliuleta mzabibu kutoka misri ukawafukuza mataifa ukaupanda, uangazishe uso wako nasi tutaokoka. 1b) Nao uliyaeneza matawi yake yake hata baharini, na vichipukizi vyake hata baharini. 2a)Ewe Bwana kwa nini umezibomoa kuta zake wote wanao pita kwenye njia wanauchuma, uangazishe uso wako nasi tutaokoka. 2b)Hata nao nguruwe wa mwituni wanauharibu kweli na wanyama wa mwituni Bwana wautafuna. 3a) E Mungu wa majeshi, twakusihi tugeukie toka juu tazama na uone uujalie, uangazishe uso wako nasi tutaokoka. 3b)Mche na mzabibu ule kweli Bwana uliopanda ni mkono wako wa kuume uliopanda. 4a) Basi hatukuachi kwa kurudi kurudi nyuma kweli hutuhuishe nasi tutakusifu, uangazishe uso wako nasi tutaokoka. 4b)Ewe Mungu Mwenyezi Mungu wa majeshi uturudishe na kwa wema utuangalie tuokoke.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa