Maneno ya wimbo
Kiitikio:
Sheria yako Bwana naipenda sheria yako Bwana, Sheria yako Bwana naipenda naipenda mno ajabu x2
Maimbilizi:
1.Bwana ndiye aliye fungu langu nimesema kwamba nitayatii maneno yako, sheria ya kinywa changu ni njema kwangu, kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
2. Nakuomba fadhili zako ziwe faraja kwangu sawasawa na ahadi yako, rehema zako zinijie nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha kwangu.
3. Ndio maana nimeyapenda maagizo yako kuliko dhahabu iliyo safi, maana nayaona mausia yako kuwa ya adili, kila njia ya uongo naichukia.
4. Shuhuda zako ni za ajabu ndio maana roho yangu imezishika, kufafanusha maneno yako kwatia nuru, kwatia nuru kumfahamisha mjinga.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu