Mtunzi: A. J. Msangule
> Tazama Nyimbo nyingine za A. J. Msangule
Makundi Nyimbo: Juma Kuu
Umepakiwa na: Geofrey Magova
Umepakuliwa mara 2,049 | Umetazamwa mara 4,674
Download Nota Download MidiBY MSANGULE A.J.
Tumwabudu Yesu katika msalaba
Tupige magoti kwa heshima na toba
Twende tunyenyekee mbele ya msalaba
Tumwabudu mwana wake Baba yeye aliye kiini cha ukombozi wetu
1. Yesu msalabani kateswa vikali kamwaga damuye ili atukomboe, nasi tuuheshimu mti wa msalaba palipo tolea sadaka yake kuu
2 Tunachokiabudu si mti pekee bali Yesu mkombozi juu ya msalaba, yeye aliyesema nikiinuliwa juu ya msalaba nitawaita wengi
3. Twende tumpelekee nazo dhambi zetu zisulibiwe zife na zizikwe naye, atakapofufuka atuumbe upya tufanane na mwili wake wa utukufu