Ingia / Jisajili

Ninakuabudu Mungu Wangu

Mtunzi: Abel T. Msigwa
> Mfahamu Zaidi Abel T. Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Abel T. Msigwa

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: ABEL MSIGWA

Umepakuliwa mara 380 | Umetazamwa mara 729

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
NINAKUABUDU MUNGU WANGU


1. Ninakuabudu Mungu wangu, unayejificha altareni, ninakutolea moyo wangu, usiofahamu siri yako.

2. Mafahamu yangu yadanganya, yanapokuona na kugusa, Namsadiki Yesu hadanganyi, yeye Mungu Mwana na Ukweli.

3. Waficha Umungu, msalabani, na ubinadamu altareni, Nami naungama zote mbili, kama mwivi yule mwenye toba.

4. Thomas aligusa majeraha, nami nasadiki bila shaka, Ewe Yesu nipe pendo lako, tumaini kwako na imani.

5. Umeteswa nini Bwana mwema, kwa kunipa mkate wa uzima, Yesu unifiche ndani yako, ili nilionje pendo lako.

6. Yesu Pelikane nitazame, na kwa damu yako nitakase, Tone moja ndilo linatosha, na dunia yote yaokoka.

7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo, atafumbuliwa kwangu lini? Nikuone Yesu uso wako, nishiriki nawe heri yako. AMINA.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa