Maneno ya wimbo
Twendeni wa amani, ndugu twendeni kwa amani; twendeni kwa amani, misa yetu imekwisha x2
Tunatumwa tukaitangaze injili yote tuliyosikia, na tena tukausambaze upendo kwao ndugu hata majirani. Twendeni kwa amani misa yetu imekwisha x2
1. Tukaitangaze injili ya Yesu kwa matendo yetu, ili wote wapate kumjua Mungu, waokolewe, twende.
2. Tuishi maisha ya mwanga na chumvi, vijijini mwetu, tushirikishane upendo halisi wake mwenyezi, twende
3. Tuwakirimie wanaohitaji kwa hali na mali, tuishi ukristo bila unafiki, tuwe wa kweli, twende
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu