Maneno ya wimbo
1a} Uhai ni pumzi yake Bwana Mungu Muumbaji,
b} Tunu ya thamani iliyopo juu ya nchi.
(Ni Neema Takatifu apewayo mtu, ili aishi mema ya Mungu duniani ×2)
2a} Kulinda Uhai (wangu) ni jukumu langu Mkristo,
b} Kutetea haki (ya ku)ishi ndio wangu wito.
(Kuhifadhi vyema mwili dhidi (ya) mauti, na kupambana vita dhidi ya dhambi na uovu ×2)
3a} Twayalilia ma(ma---)isha twabeza uhai,
b} Kwa shingo twakaza(za---) vichwa kubeba kiburi.
(Twasahau Neema Kuu kuto(ka) kwa Mungu, huku kwa visu nazo sumu twafyeka yake pumzi ×2)
4a} Uovu watama(ma---)laki dhambi yafurika,
b} Wanadamu wame(me---)asi, wakana uzima.
(Wakiipinga sheria yake (-ke) Mungu Mkuu, wakifuata haja ya tamaa za ulimwengu ×2)
5a} Mauaji yasha(sha---)miri damu yazizima,
b} Nchi zachinja wa (wa---)toto kwa watu wazima.
(Wanadamu wakataa kuli(nda) uhai, waharibu vizazi wasishiriki uumbaji ×2)
6a} Kwa unyekevu (mkubwa) twakuomba msamaha,
b} Ukainusuru (ru---) aridhi yenye hatia.
(Urudishe tena hofu yako (du)niani, mpaka mataifa wakutambue Mungu wa Haki.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu