Ingia / Jisajili

Umuhimu Wa Sakramenti Ya Ndoa

Mtunzi: Justine Mgobela
> Mfahamu Zaidi Justine Mgobela
> Tazama Nyimbo nyingine za Justine Mgobela

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Ndoa

Umepakiwa na: Justine Mgobela

Umepakuliwa mara 8 | Umetazamwa mara 16

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Tutambue "UMUHIMU WA SAKRAMENTI YA NDOA" ili tuishi katika familia zetu kwa pendo la Mungu;

Mt.Paulo anatuhimiza sakramenti ya ndoa hutuletea Baraka takatifu ya Mungu asili ya pendo lake;

Wakristo tuache uchumba sugu kwa maana mume asiyeamini hutakaswa katika mke wake, kwa maana mke asiye amini hutakaswa katika mume wake;

Kila mwanaume awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe, shetani asije kutujaribu kwa kutokuwa na nafasi kwetu;

Familia takatifu ni familia yenye Baraka, hiyo ndiyo familia bora yenye misingi ya kikristo, Hiyo hudumu katika, katika pendo la Mungu, watoto ndani ya nyumba huwa na malezi bora;

"UMUHIMU WA SAKRAMENTI YA NDOA"

1.Iwe chachu ya upendo,

2.Iwe chachu ya furaha,

3.Iwe chachu ya Amani;

Na ahimidiwe Baba wa Bwana wetu Yesu kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote kwa maana ndiye atufanyaye kuwa imara;

Tumwamini kristo awe ndani yetu tupate kudumu ndani ya pendo lake;

Wakristo wote tunapaswa kutambua kwamba, Ndoa ni ya mke mmoja (pia) ndoa ni ya mume mmoja.



Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa