Ingia / Jisajili

Unifanye Chombo Cha Amani

Mtunzi: Zacharia Gerald
> Tazama Nyimbo nyingine za Zacharia Gerald

Makundi Nyimbo: Anthem | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Innocent Nuluva

Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 0

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

UNIFANYE CHOMBO CHA AMANI

UTANGULIZI

Bwana Mungu ukiniuliza,
Ninataka nini, natamani nini,
Ombi langu kwako ni moja tu,
Ninaomba leo, nakuomba Bwana.

KIITIKIO

Unifanye chombo cha amani yako,
Bwana wangu, Bwana, ee Bwana,
Ee Bwana, unifanye chombo cha amani yako,
Na hiyo ndiyo sala yangu, ee Mungu.

Kiitikio kinarudiwa kulingana na alama za marudio kwenye noti, na mwisho wake una maneno “Ee Mungu milele.”

MASHAIRI

1. Ubeti wa kwanza

Palipo chuki nilete mapendo,
Penye makosa nilete nisamaha,
Penye mashaka nilete imani,
Ndipo moyo wangu utafurahi, Bwana.

2. Ubeti wa pili

Pasipo matumaini niyalete,
Palipo na giza nilete mwanga,
Penye huzuni nilete furaha,
Ndipo moyo wangu utafurahi, Bwana.

HITIMISHO

3. Ubeti wa tatu

Ee Bwana unisaidie,
Nami ninatamani sana,
Kufariji kuliko kufarijiwa,
Ninatamani kufahamu kuliko kufahamiwa,
Ninatamani kupenda kuliko kupendwa.

Kwa kuwa ni katika kutoa ndipo tunapokea,
Tukisamehe ndipo tunasamehewa,
Ni katika kifo ndipo tunazaliwa,
Katika uzima milele, milele.
Amina.



Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa