Mtunzi: Joseph D. Mkomagu
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph D. Mkomagu
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 8,259 | Umetazamwa mara 15,248
Download Nota Download Midi
Uniponye roho yangu ee Bwana, kwa maana mimi nimekutenda dhambi x 2
Adui zangu wananisema kwa maneno mabaya, wanasema atakufa lini, jina lake likapotea x 2
1. Heri amkumbukaye mnyonge, Bwana atamwokoa siku ya tatu, Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, naye atafanikiwa katika nchi.
2. Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani, katika ugonjwa wake, umemtandikia, name nalisema Bwana unifadhili, uniponye roho yangu, maana nimekutenda dhambi.
3. Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza, umeniweka mbele za uso wako milele,
na atukuzwe Bwana Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele amina amina.