Mtunzi: John Sway
> Mfahamu Zaidi John Sway
> Tazama Nyimbo nyingine za John Sway
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 758 | Umetazamwa mara 2,826
Download NotaUSIKATE TAMAA
KIITIKIO
Katika taabu na mateso, Katika shida na magonjwa usikate tamaa (bali umtumaini Mungu tena umtegemee yeye kwani ndiye muweza wa yote X2.
Mashairi:
1. Mkumbukeni mtumishi wa Mungu mtumishi wa Mungu Ayubu aliteseka na kujaribiwa sana lakini hakukata tamaa bali alimtegemea Mungu.
2. Mkumbukeni na Bwana wetu Yesu Bwana wetu Yesu Kristu aliteseka na kujaribiwa sana lakini hakukata tamaa bali alimtegemea Mungu
3. Tunapopatwa na shida na magonjwa majaribu mengi ya kutisha tusiogope tumtumaini Mungu pasipo kukata tamaa, Mungu hashindwi na jambo lolote