Ingia / Jisajili

Wapenzi Wana Harusi

Mtunzi: Stanslaus Mujwahuki
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Mujwahuki

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: Gervas Kombo

Umepakuliwa mara 3,850 | Umetazamwa mara 8,439

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  1. Wapenzi wana harusi, salamu twawatolea,
    Kwa kuwa mnaingia katika maisha mapya,
    (Yale mliyongojea kwa siku zilizopita, ndoa ni msalaba tunayajua yakini) x 2
     
  2. Mbali kidogo mwaenda, wawili sio watatu,
    Ndivyo ilivyo sheria itendekavyo daima,
    (Waume ndio mababa, alivyoandika Mungu, ndoa ni msalaba tunayajua yakini) x 2
     
  3. Sote tunafurahia, kwa shangwe yenye utii,
    Rabeka mke itika uitwapo na mumeo,
    (Nawe mume itika uitwapo na mke, ndoa ni msalaba tunayajua yakini) x 2
     
  4. Wapenzi wana harusi, kwa heri twawaageni,
    Mpendane ninyi vyema katika maisha yenu,
    (Mungu awajalieni, baraka neema na nguvu, ndoa ni msalaba tunayajua yakini) x 2

Maoni - Toa Maoni

Francis Aug 23, 2016
Tunawashukuru kwa kutuwezesha kupata nyimbo za matukio mbalimbali zikiwa katika music wake noted songs

Toa Maoni yako hapa